Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema CCM Zanzibar kupitia rasimali zake inatarajia kuanza kuwalipa posho kila mwezi Mabalozi kwa ngazi ya Shina.
Baada ya mwendelezo wa rasilimali za uwekezaji na Chama kujitegemea kwa kuimarika kiuchumi Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar Dk. Mwinyi ametoa ahadi pia kuwalipa na watendaji kwa ngazi zote za chini.
Ameyasema hayo tarehe 11 Juni 2023 ukumbi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja alipokuwa akizungumza na Viongozi wa CCM ngazi ya Shina, Wajumbe wa Halmashauri Jimbo, Wilaya na Mkoa.