Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani (African Geoporitical Group in the IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Duarte Pacheco, wakati alipomtembelea katika Ofisi ndogo za Rais huyo zilizopo katika ukumbi wa Grand Mogador Menara Marrakesh, nchini Morocco leo tarehe 14 Juni, 2023.
Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia amemueleza Rais huyo anayemaliza muda wake wa Uongozi kuhusu nia yake ya kugombea nafasi ya Urais wa IPU kwa mwaka 2023-2026 unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu katika Mji wa Luanda Nchini Angola.
Rais Pacheco amemtakia kila la kheri Dkt. Tulia katika kuelekea kwenye uchaguzi huo na kumtaka kuendeleza mashirikiano ya kuiunganisha dunia endapo atapata nafasi hiyo kama ambavyo amekuwa Kiongozi wa mfano tangu achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja huo.
SUBSCRIBE KWENYE YOUTUBE CHANNEL YETU