Club ya Real Madrid ya Hispania imetangaza kumsajili Kiungo wa Kimataifa wa England Jude Bellingham (19) kwa Mkataba wa miaka sita kutokea Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Bellingham anatajwa kusajiliwa kwa dau la pound milioni 88.5 na atatambulishwa rasmi Alhamisi ya June 15 2023.
Jude Bellingham alizaliwa June 29 2003 Stourbridge Englanda alianza kucheza soka la vijana katika academy ya Birmingham City 2010-2019 na Timu za Taifa za vijana za England kuanzia 2016 U-15, U-16, U-17 & U-21.
SUBSCRIBE KWENYE YOUTUBE CHANNEL YETU