RAIS wa Yanga, Injinia Hersi Said, amepiga mkwara mzito kuhusu masuala ya usajili akiweka wazi kuwa jina lolote atakalopewa atafanyia kazi kuhakikisha anamleta mchezaji huyo.
Injinia Hersi alifanikisha madili ya wachezaji wengi ndani ya kikosi cha Yanga akiwemo Stephane Aziz KI ambaye alikuwa anakipiga ASEC Mimosas ya Ivory Coast.
Aziz Ki alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Simba pamoja na Azam FC, jambo lililoongeza presha kwenye kuisaka saini yake na mwisho aliibuka Yanga.
Injinia Hersi amesema: “Kwenye suala la usajili, Yanga tupo tofauti na tunazidi kuiboresha sekta hii kutokana na kuwa na mfumo wa mabadiliko, hivyo wakishafanya mchakato wao ninawaambia tu jina lolote wanipe.
“Wakinipa jina la mchezaji ambaye wanamuhitaji popote kule hizo ndizo kazi zangu, nitahakikisha ninakamilisha hilo dili na kuwapatia mchezaji wao.”