Wabunge wa Afrika Kusini siku ya Jumanne walipiga kura kuunga mkono mswada wenye utata ambao unalenga kutoa huduma za afya bure kwa wote lakini wakosoaji wanahofia kwamba haiwezi kuwa endelevu.
Mfuko utakaoanzishwa chini ya sheria ambao bado unapaswa kupitishwa na bunge kuu kabla ya kusainiwa kuwa sheria na Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa, utatoa huduma za afya kwa wote kwa viwango vitakavyoamuliwa na serikali.
Baada ya mjadala mkali mswada huo ulipitishwa na wabunge 205 na kukataliwa na wabunge 125. Waziri wa Afya nchini humo, Joe Phaahla alielezea kupitishwa kwa muswada huo ambao umekuwa ukiandaliwa kwa miaka 12 kama hatua ya kihistoria na moja ya vifungu vya sheria vya mapinduzi tangu kumalizika kwa ubaguzi wa rangi nchini humo.
Bima ya Afya ya Taifa (NHI) itakuwa mfumo wa huduma za afya ulio sawa, unaopatikana, kwa gharama nafuu, na ulioimarishwa.
SUBSCRIBE KWENYE YOUTUBE CHANNEL YETU