Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump Jumanne alasiri alifika mbele ya hakimu wa mahakama ya serikali kuu mjini Miami, Florida, amekanusha mashtaka ya kuhifadhi kinyume cha sheria mamia ya nyaraka za siri za serikali baada ya kuondoka Ikulu, na kuzuia juhudi za serikali kuzipata.
Trump aliweka historia wiki iliyopita wakati jopo la mahakama lilipomshtaki kwa makosa 37 ya uhalifu, yakiwemo makosa 31 ya kuhifadhi kwa makusudi taarifa za siri za ulinzi wa taifa, huko Mar-a-Lago, katika makazi yake kwenye jimbo la Florida.
Kushtakiwa kwa rais huyo wa zamani kulifanyika chini ya ulinzi mkali, huku mamia ya wafuasi wa Trump walikusanyika nje ya mahakama.
Mchambuzi wa siasa za kimataifa David Monda ambaye anaanza kwa kuelezea umuhimu wa kesi hii iliyogonga vichwa vya habari kitaifa na kimataifa.Trump alikuwa ametoa wito kwa wafuasi wake kuandamana huko Miami, akizua wasiwasi kwamba mkusanyiko huo unaweza kugeuka ghasia. Lakini kesi mahakamani hazikuwa na matukio yoyote makubwa.
SUBSCRIBE KWENYE YOUTUBE CHANNEL YETU