Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewateua Viongozi wafuatao kuwa na Hadhi ya Balozi:-
1. Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi,
2. Dkt. Salim Othman Hamad, Msaidizi wa Rais anayeshughulikia masuala ya Siasa na,
3. Dkt. Kassim Mohamed Khamis, Msaidizi wa Rais anayeshughulikia masuala ya Hotuba.
Aidha, Vyeo walivyonavyo vinabaki kama vilivyo. Uteuzi huu wa Hadhi ya Balozi umeanza tarehe 12 Juni, 2023.
Wateule wataapishwa tarehe 16 Juni, 2023 kuanzia saa 04:00 asubuhi – Ikulu, Chamwino – Dodoma.
SUBSCRIBE KWENYE YOUTUBE CHANNEL YETU