Na Evelyne Ernest
WAKAZI wa kata ya Kashai manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, wameshitushwa baada ya mwanaume mmoja kukamatwa akichinja mbwa ambaye ambaye haikufahamika nyama ya mbwa huyo ilikuwa inaipeleka wapi.
Akizungumza na Divine FM, Diwani wa kata hiyo Ramadhan Kambuga amesema tukio hilo limefanyika siku ya jumanne, wakati mwanaume huyo akichinja mbwa katika eneo la kahororo na kwamba alikutwa akitafuna nyama ingine ikiwa mbichi.
Ameongeza kuwa mtuhumiwa amefikishwa kituo cha polisi kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi na kuwataka wananchi kuacha tabia ya kununua nyama mitaani, na badala yake wanunue katika maduka.
Baadhi ya wananchi na wakazi wa kata hiyo wamesema vijiwe vya kuuza mishikaki katika kata hiyo vimeongezeka na kuiomba serikali kuwakagua watu wote wanaojiusisha na uuzaji wa mishikaki ili kujiridhisha kama wana uthibitisho na vibali na pia kujihakikishia kama nyama inayouzwa huko ina mihuri ya mamlaka husika.