Wakati Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikisoma bajeti ya Sh2.8 trilioni kwa mwaka wa fedha 2024, baadhi ya wananchi wamekuwa na maoni tofauti.
Wakizungumza baada ya kusomwa kwa bajeti hiyo, wananchi hao akiwemo Ameir Juma, mkazi wa Unguja amesema kwa kiasi fulani imezingatia matakwa ya wananchi wa kawaida.
“Tunaona kwenye sekta ya afya, elimu na maji kuna maendeleo makubwa na mikakati imetajwa,” alisema Juma.
Naye Fatma Said alipongeza kuondoshwa kwa stempu duty jambo ambalo lilikuwa ni kilio cha muda murefu.
Akizungumzia kuongeza kwa malipo ya Sh100 katika mafuta ya dizeli na petroli, Haji Muhmed alisema kunaweza kuleta shida kwa sababu mafuta ya kupanda kila kitu kitapanda.
“Kikubwa nilichofurahi ni hiyo kodi ya stempu, imelikuwa inaleta shida kwa wafanyabiashara, kuondolewa kwake kutaleta ahueni kwa wananchi,” alisema Burhan Said mfanyabaishara mwingine kutoka Unguja.
Akisoma mwelekeo wa bajeti ya Serikali Kuu katika Baraza la Wawakilishi Chukwani leo Alhamisi Juni 15, 2023, Waziri wa Fedha, Dk Saada Mkuya amesema fedha hizo Sh1.3 trilioni ni kazi za kawaida na Sh1.5 trilioni mpango wa maendeleo.
“Sh1.4 bilioni misaada na mikopo kutoka kwa Washirika wa Maendeleo Sh686.61 bilioni, mikopo ya ndani nje kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo Sh717.21.
Kati ya mapato hayo, mapato ya ndani ni Sh1.4 bilioni, misaada na ikopo kutoka kwa Washirika wa Maendeleo Sh686 bilioni, mikopo ya ndani na nje kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo Sh717.21 bilioni,” alisema
Akitaja vipaumbele hivyo ni pamoja na ujenzi wa barabara eneo hili litahusisha ujenzi wa barabara kuu, barabzra za mjini, barabara za ndani na vijijini zenye urefu wa kilomita 782.1 kilomita ambazo zitagharimu Sh373.5 bilioni.
Kiwango hicho ni sawa na asilimia 29 ikilinganishwa na Sh2.6 trilioni za bajeti iliyopiata mwaka 2022/23.
Kuimarisha huduma za kijamii
Eneo hili litahusisha sekta tofauti zinazohusiana na usambazaji wa huduma za jamii ikiwemo sekta elimu, afya, usambazaji wa huduma za maji serikali inatarajia kutumia Sh338.8 bilioni kutekeleza miradi mbalimbali.
Katika uimarishaji uchumi wa buluu serikali inalenga kukuza na kuimarisha matumizi endelevu ya bahari na kuwawezesha wajasiriamali kwa kuongeza thamani mazao ya baharini na kukuza mitaji yao mradi huu utatumia Sh23.5 bilioni kwa fedha za Serikali.
Alisema Zanzibar ina fursa ya kipekee katika utalii kutokana na jina, mandhari, umahiri, mazingira pamoja utamaduni wa watu wake.
Maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanayoendelea kutokea, yanalenga pamoja na mambo mengine, kuhakikisha kuwa, upekee wa Zanzibar katika taswira ya kitalii unaleta tija ya kiuchumi pamoja na maendeleo ya watu wake lakini changamoto kubwa iliyopo kwa sasa, ni kuwa ongezeko la watalii hapa Zanzibar haliakisi mapato yanayoingia Serikalini
Zanzibar kulipa wateja wa FBM
“Mwaka 2017, Benki Kuu ya Tanzania, ilisimamisha shughuli za biashara kwa iliyokuwa Benki ya FBME ambayo ilikuwa na makao yake makuu yake nchini Cyprus ilifungua tawi mjini Dar-Es-Salaam., Benki hii pia ilikuwa na Tawi hapa Zanzibar”.
Benki hii ilianza shughuli zake mwaka 2003.
Mwaka 2014, Benki hii iliwekwa chini ya uangalizi wa Benki Kuu ya Tanzania na 2017, ikawa chini ya ufilisi wa bodi ya bima za Amana (DIB).
Wakati inawekwa chini ya ufilisi mwaka 2017, idadi ya wateja walikuwa ni 6,600 ambapo wateja wa Zanzibar ni 2,329 ambao wanadai Sh20,5 bilioni
Hata hivyo, kwa kuwa hadi sasa, kesi baina ya DIB na Mamlaka za Cyprus ambako pia kuna amana za FBME inaendelea, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imeamua kulipa amana za wateja wa iliyokuwa FBME kwa upande wa Zanzibar.
“Serikali, itaanza mchakato huo, baada ya kukamilika taratibu ambazo itazitangaza baadae,” alisema
Alisema uchumi wowote wa nchini, pamoja na mambo mengine, unategemea kwa kiasi kikubwa uwekezaji ambao utaleta tija kupitia kuzalisha ajira za wananchi wake na hivyo kupatikana kwa kodi ambayo itawezesha utekelezaji wa miradi na shughuli nyingine za nchi.
Alisema changamoto kubwa imekuwa ni upatikanaji wa mitaji kwa mahitaji ya uwekzaji hivyo serikali kunazisha benki hiyo.
Kuongeza pensheni jamii ambapo itasiwmaiwa kwa kupitia benki kutoka Sh20,000 hadi Sh50,000.
Punguzo la ushuru wa stempu
Kumekuwapo na malalamiko ya wafanyabiashara kulipa kodi ya mapato inayokusanywa na TRA na Ushuru wa Stempu unaokusanywa na ZRA,
Alisema ili kuondoa changamoto hiyo na kurahisisha biashara na ulipaji kodi wa hiari, Serikali inapendekezwa kufuta utozwaji wa kodi inayokusanywa na TRA na ZRA kwa mfanyabiashara mmoja badala yake kuanzisha kodi mpya itakayaitwa Ushuru wa Mauzo Ghafi.
Pia, alisema Serikali inapendekeza kuanza kutoza ushuru wa bidhaa kwa asilimia 30 kwa waagizaji wa Electronic Cigarette na shisha.
Lakini inapendekeza kurudisha kiwango cha awali cha Sh100 kwa lita ya mafuta ya Dizeli na Petroli kutoka Sh50 ya kiwango cha sasa.