Na Bukuru Daniel – Burundi
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Burundi cha CNL mbunge Agathoni Rwasa amewafukuza watu kumi na moja katika uongozi wa chama hicho kwa shutuma za makosa mbali mbali.
Katika waraka ambao ameweza kuuweka hadharani,Agathon Rwasa anasema kuwa viongozi hao wamekiuka kanuni na taratibu za chama hicho ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua mbali mbali ndani ya chama bila idhini yoyote.