Tafiti za kisayansi kuhusu viumbe hai zinaeleza kuwa, Malkia wa nyuki ambaye hajawahi kukutana na dume (bikra) akiwa tayari kupata kizazi kuhitaji dume (drone honey bee), hupaa kuelekea sehemu yalipo madume, hapo hukutana na dume la kwanza ambalo akijamiiana nalo.
Sehemu za siri za dume hilo hubaki kwa malkia ili kurutubisha mayai ya malkia, kitendo cha sehemu za siri za dume kubaki kwa malkia hupelekea tumbo la dume huyo kupasuka na kufa muda mfupi baada tu ya kujamiiana na malkia.
Baadaye huja dume jingine ambalo nalo huzitoa sehemu za siri za dume la kwanza kisha naye kumpanda malkia, vivyo hivyo na kwa (drone honey bee) wengine watakaofuata.
Malkia anao uwezo wa kujamiiana na madume 7 hadi 10. Nyuki malkia anao uwezo wa kutunza mbegu za kiume zaidi ya milioni 100 kwenye mirija yake ya uzazi.
Ni mayai milioni 5 mpaka milioni 6 pekee ndiyo huyatunza kwenye (mfuko wa mayai baada ya kujamiiana) spermatheca na haya hutumika kurutubisha mayai yake polepole (kwa awamu) na kupata watoto katika maisha yake yaliyosalia.
Mayai yaliyorutubishwa hutoa nyuki malkia na wafanyakazi wa kike, mayai ambayo hayajarutubishwa hutoa madume kwa ajili ya kujamiiana na malkia pekee (drone honey bee), ambao hawawezi hata kula mpaka wapate msaada wa kulishwa.
Malkia wapya (atakaowazaa) nao watakutana na madume, hupata watoto na kutengeneza makonoli yao. Nyuki wafanyakazi wa kike hawajamiiani, lakini wanao uwezo wa kutaga mayai ambayo hayajarutubishwa na kutoa nyuki dume (drone honey bee).
Baada ya malkia kutaga mayai yake, nyuki wafanyakazi wanao uwezo wa kuhisi na kutambua, huyazungushia mayai hayo mafuta kwa ajili ya kuyalinda (kuyakinga na maadui) lakini pia ni chakula kwa malkia na viumbe hao baada ya kuzliwa.
Mayai yatakayotoa nyuki wa kiume na wafanyakazi huzungushiwa mafuta ya kawaida lakini yale yatakayotoa malkia huzungushiwa mafuta maalum (royal jelly). Malkia anahitaji siku 16 tu kukomaa (to be matured), majike (wafanyakazi) huhitaji siku 21 na madume huhitaji siku 24 tu.