Wananchi wa Ufaransa pamoja na watalii wanaoitembelea nchi hiyo wanaugulia maumivu baada ya kung’atwa na kunguni ambao wamesambaa katika maeneo mengi hasa ya umma.
Kufuatia kuwepo kwa picha mbalimbali za video mitandaoni zikionyesha kuwepo kwa wadudu hao hasa katika jiji la Paris kwenye treni za mwendokasi, hospitali, nyumba za sinema na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Charles-de-Gaulle, serikali ya Ufaransa imesema inaelekeza juhudi zake katika kupambana na kunguni hao.
“Jimbo linahitaji haraka kuweka mpango wa utekelezaji dhidi ya janga hili wakati Ufaransa inajiandaa kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki na Paralympic 2024,” ameandika Naibu Meya wa Paris, Emmanuel Gregoire katika barua yake kwa Waziri Mkuu Elisabeth Borne.