Zaidi ya watu elfu moja wamefariki dunia nchini Bangladesh, kufuatia mlipuko wa homa ya Dengi (Dengue Fever).
Taarifa kutoka mamlaka za afya nchini Bangladesh zimeeleza kuwa takwimu hizo ni katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari, 2023 hadi sasa ambapo kati ya watu hao waliofariki dunia watoto ni 100.
Katika kipindi hicho cha watu 20,800 wameugua homa ya Deingi nchini Bangladesh.
Mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo kuongezeka kwa joto kunatajwa kusababisha ongezeko la maambukizi ya homa hiyo ya Dengi.