Bernardo Silva amedokeza kuwa anaweza kujaribu kumshawishi Joao Neves mwenye umri wa miaka 19 ajiunge na Manchester City licha ya Manchester United kumtaka kiungo huyo wa Benfica. (MEN)
Kiungo wa kati wa Ureno Ruben Neves, 26, hatarajiwi kuondoka katika klabu ya Saudi Pro League Al-Hilal mwezi Januari kutokana na kuhusishwa na Newcastle United. (Subscription Required)
Kiungo wa kati wa City na Ureno Silva, 29, anasema angependa kurejea kuichezea Benfica kabla ya kumaliza soka yake. (CNN, via TalkSport)
Meneja wa Manchester United Erik ten Hag hatamruhusu mlinzi wa kati Mfaransa Raphael Varane, 30, kuondoka katika klabu hiyo hadi dirisha la usajili la majira ya kiangazi litakapomalizika. (Sun)
Juventus wana matumaini kwamba mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic mwenye umri wa miaka 23 atakubali kusaini mkataba wa nyongeza katika klabu hiyo licha ya kumtaka Arsenal na Manchester United. (90min)
Chelsea wanatumai kuwa wataweza kumuuza mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku msimu ujao wa joto, huku Roma wakitamani kufanya uhamisho wa mkopo wa mchezaji huyo wa miaka 30 kuwa wa kudumu. (Evening Standard)
Mshambulizi wa Ufaransa Antoine Griezmann hatajiunga na Manchester United na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 analenga tu Atletico Madrid. (Fabrizio Romano)
Fulham itamruhusu kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha, 28, kuondoka na kujiunga na Bayern Munich Januari kwa chini ya euro 60-65m (£52m-£56m) ambayo klabu ilitaka hapo awali. (Florian Plettenberg, Sky Germany)
Kipa wa Uhispania David de Gea ameweka wazi kuwa hataki kujiunga na klabu ya Saudi Pro League lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 anaweza kuhamia Ligi Kuu ya Soka mnamo 2024. (90min).
Bayern Munich wanashinikiza kumsajili beki wa Japan Takehiro Tomiyasu msimu ujao wa joto lakini Arsenal hawataki kumwachia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Florian Plettenberg, Sky Germany)
Baadhi ya wachezaji wa Manchester United wanaamini mwanzo mbaya wa timu hiyo msimu huu ulisababishwa na meneja Erik ten Hag kukifanyisha kikosi kazi kupita kiasi katika maandalizi ya msimu mpya. (Guardian)
Kiungo wa kati wa Liverpool Mhispania Thiago Alcantara, 32, ni miongoni mwa chaguzi ambazo Barcelona wanaweza kuzingatia wanapotafuta kuchukua nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Gavi, 19, aliyejeruhiwa. (90min)
Kiungo wa kati wa Tottenham na Argentina Giovani lo Celso, 27, pia amejitokeza kama chaguo la mkopo kwa Barcelona, ambao hawana uwezekano wa kutafuta mbadala wa kudumu wa Gavi licha ya kupokea fidia ya hadi pauni milioni 6 kutoka Fifa kufuatia jeraha lake kwenye majukumu ya kimataifa. (Mail)
Arsenal wanaweza kumruhusu kiungo wa kati wa Ureno Fabio Vieira, 23, kujiunga na klabu ya Ufaransa ya Marseille kwa mkopo. (Mirror)
Beki wa kati wa Juventus na Brazil Gleison Bremer, 26, anasema ana nia ya kucheza katika Ligi ya Premia. (Telegraph – usajili unahitajika)
FA inasema iko tayari kukagua ushahidi wa uwezekano wa ukiukaji mkubwa wa sheria za mawakala katika uhamisho unaohusisha Tottenham Hotspur, Portsmouth na Jermain Defoe. (Time – Subscription Required)
Liverpool wanaongoza harakati za Ligi Kuu ya Uingereza kutatua kesi ya Manchester City ya haki ya kifedha. (Football Insider)