Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Murshid Ngeze amewataka Wenyeviti wa Halmashari pamoja na Wakurugenzi nchini kuacha tabia ya kuvutana kwani jambo hilo linakwamisha maendeleo ya Wananchi badala yake watumie muda huo kusimamia kakamilifu miradi ya maendeleo inayoletwa na serikali ikamalike kwa wakati.
Akizungumza na vyombo vya habari Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera amesema kuna baadhi ya Halmashauri zinakosa maelewano ya viongozi hao jambo ambalo linapelekea kuwagharimu wananchi.
Mwenyekiti Ngeze amesema katika Halmashauri zetu utakuta inaibuka migogoro ya viongozi na watumishi huku akitolea mfano wa Mkoani Morogoro Waziri wa TAMISEMI, aliitisha kikao cha ndani cha :Wakurugenzi wote wa Mkoa huo na wenyeviti wa Halmashauri, Meya, Wakuu wa Wilaya na Maafisa Tawala na Viongozi wengine, ili kuzungumzia mivutano na inayoathiri utendaji kazi na kwenye mkutano wa ALAT Zanzibar alikemea jambo hilo.
“inafika hatua Mwenyekiti na Mkurugenzi wanavutana Halmashauri itakwendaje, Matokeo yake utakuta miradi ya maendeleo haiendi na miradi vipolo haiendi huku Kuna uvunjifu wa fedha kwa sababu hakuna mshikamano wa utendaji kazi,” alisema Ngeze.