MBUNGE wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye ameutahadharisha Umma wa watanzania kwamba hana akauti yoyote ya mtandao wa kijamii inayofanya kazi kwa sasa (iliyo-active).
Nape amelazimika kutoa ufafanuzi huu kutokana na kuibuka kwa akaunti hasa katika mtandao wa X zinazoandika vitu mbalimbali zikiwa na jina la Nape Nnauye na kufanya kama ni yeye amezungumza au kutoa maoni yake, kitu ambacho amesema sio kweli na kusisitiza kuwa hausiki nazo.