Msaidizi wa rais wa Urusi Yuri Ushakov alisema Jumatatu kwamba Moscow haiko tayari kufanya mazungumzo ya amani na Ukraine kwa sasa kutokana na mashambulizi ya Kyiv katika eneo la Kursk la Russia, lakini kwamba Urusi haiondoi mapendekezo yake ya awali ya amani.
Ushakov alitoa maoni hayo katika taarifa ya video iliyotangazwa na chombo cha habari cha SHOT.
“Katika hatua hii, kwa kuzingatia mradi huu (Kursk), hatutazungumza,” Ushakov alisema.
Uvamizi wa ghafla wa Ukraine, ambao ni mkubwa zaidi nchini Urusi na mataifa ya kigeni tangu Vita vya Pili vya Dunia, ulianza Agosti 6 wakati maelfu ya wanajeshi wa Ukraine walipovuka mpaka wa magharibi wa Urusi katika aibu kubwa kwa jeshi la Urusi.