Mchezo wa Marudiano wa hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya wenyeji, Yanga dhidi ya Vital’O Fc ya Burundi utachezwa katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi na sio Benjamin Mkapa kutokana na marekebisho yanayoendelea kwa sasa katika Uwanja wa Mkapa.