Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Chief Kingalu katika Manispaa ya Morogoro leo Agosti 23, wamegoma kufungua biashara zao na kufinga barabara wakidai serikali ichukue hatua za kuwaondoa akinamama wanaopanga biashara barabarani kwani wanasababisha wateja kutoingia kabisa ndani ya soko kununua bidhaa.
Mwenyekiti wa soko hilo, Khalid Mkunyagela, amesema kuwa changamoto hiyo imepelekea wateja kushindwa kuingia sokoni kununua bidhaa, hali inayosababisha biashara ndani ya soko kukosa wateja.
“Kwa hali iliyofikia inaonekana tunazidi kuonewa kila kiongozi anaekuja anakuja na matamshi yake,leo hii sisi tunapambana na kazi ngumu kuwataka watu watoke barabarani anakuja kiongozi mwingine anasema watu warudi barabarani masoko yafungwe je ili jengo kubwa lililojengwa kodi italipwa na nani na wafanyabiashara waliopo kipato watakipata wapi watu wameekeza,” alisema Mkunyangela.
Naye Japhet Dickson mfanyabiashara wa soko la kilangalu amesema,wamefanya mgomo huo sababu kuu ikiwa ni kauli ya mkuu wa wilaya Musa Kilakala kuwataka wakinamama wanaoiza mboga kurudi kufanya biashara katika eneo ambalo wamachinga walitolewa na kupewa vizimba na mkuu wa mkoa wa zamani Albert Mando.
“Mahali hapa kilichotokea ni kwamba siku ya juzi mkuu wa wilaya alitamka kwamba wauza mbonga wote wa mkoa wa moro waweze kuuza nyanya zao eneo hilo la hapo Islam ambapo sisi wamachinga zamani tulikua tunauzia zamani akaja Albert Mando akatutoa akatuleta katika la chief kingalu matokeo yake tunashangaa mkuu wa wilaya aliyekuja anaruhusu wamama warudi tena barabarani jana tumeshida soko limelala akuna wateja” alisema Dickson
Naye Batuli Ibrahim mfanyabiashara Soko la Kingalu amesema,wanategema biashara zao kupata fedha ya kuwasomesha watoto wao hivyo kuruhusiwa kwa wafanyabiashara wengine kwenda kupanga bishara zao barabarani kutahadhiri uwepo wa wateja katika soko hilo hivyo wanaomba kupata kauli ya mkuu wa wilaya juu ya swala hilo.
“Leo tumeamua kufunga biashara zetu kutokana na kauli ya mkuu wa wilaya na tumeona kwa vitendo,kwakuwa tuliskia hatukuamini lakini jana asubui tulipo amka tukaenda kutizama yale maeneo kama kweli wamepanga biashara zao,kwahiyo sisi tuliazimia kufunga soko labda soko alina umuhimu,sisi tunataka kupewa majibu kama hili ni soko tena au wamebadilisha matumizi na watupe utaratibu wa wale watu waliowaruhusu kufanya utaratibu pale sisi tunategemea soko hili kusomesha watoto wetu wateja wakikosekana mnataka tuende wapi” Alisema Batali.
Dar24 Media imefanya jitihada za kumtafuta Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Musa Kilakala ambaye amesema maelekezo aliyotoa yeye ni kutowapiga na kuwachukulia vitu vyao Wafanyabiashara na badala yake wapewe maelekezo ya wapi wafanyie niashara zao.
“Serikali ilishatenga maeneo ya watu kufanya Biashara kwahiyo haiwezekani watu wakapanga biashara barabarani na wale watu wa sokoni watauza wapi kwahiyo mimi nakuja kuzungumza nao warudi kufanya biashara zao kama kawaida, watu wasipange biashara barabarani, maelekezo niliyotoa mimi ni kwamba watu wasipigwe kwasababu kuna kasumba ya watu kuwapiga na kuwachukulia vyakula vyao waelekezwe utaratibu wanatakiwa wafanye biashara wapi sasa inawezekana kuna mtu ameleta taaruki kwa jambo ambalo alikuwa hivyo,” alisema Kilakala.