Mkaguzi kata ya Kisangura Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Mkaguzi msaidizi wa Polisi A/Insp Genuine Kimario ameendelea kuyafikia makundi mbalimbali katika kata yake ambapo ametoa viti mwendo kwa Mzee Benjamini Imori miaka 80 Mkazi wa kata hiyo na Mariam Wankuru.
Mkaguzi kimario amefikia hatua hiyo baada ya kumuona mzee huyo katani hapo akiwa anachangamoto ya kupooza katika mwili wake hali iliyosababishwa na changamoto za kiafya aliyoipata Tangu 2019 ambapo alichukua hatua za haraka kuwasaidia wananchi hao.
Aidha Mkaguzi kata hiyo amebainisha licha ya kuwa na jukum la kisheria la kuhakikisha wananchi hao wako salama wao na mali ameweka wazi kuwa anayonafasi ya kushirikiana na Jamii katika changamoto zao ili wafurahie maisha kama wananchi wengine katani hapo.
Vilevile ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wengine kuungana nae katika kuwasaidia wananchi ambao bado wana changamoto ya kupata viti mwendo katika Kata yake.
Sambamba na hilo amewaomba wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi juu ya watu wenye nia ya kufanya uhalifu na walifu ili Jeshi hilo liwachukulie hatua za kisheria.