Shirika la reli Tanzania Treni ya abiria namba Y14 ikiwa na kichwa cha treni namba 9002, mabehewa 12 ya abiria, behewa moja la vifurushu (parcel) na behewa moja la breki imepata ajali kati ya Stesheni ya Kazuramimba na Uvinza mkoani Kigoma majira ya saa 7:30 usiku tarehe 28 Agosti 2024.
Ajali imetokea baada ya mabehewa sita (6) ya treni kuacha njia na kupelekea majeruhi 70, wanawake 26 na wanaume 44. Treni ilikuwa na jumla ya abiria 571 walisafiri kutoka kigoma kuelekea mikoa ya Tabora, Dodoma, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.
TRC kwa kushirikiana na Kitengo cha Afya cha Mkoa wa Kigoma walifanikiwa kuwapeleka majeruhi katika hospitali ya Wilaya ya Uvinza kwaajili ya matibabu. Hali za afya za abiria zinaendelea kuimarika, majeruhi 57 tayari wameruhusiwa, nane wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Uvinza na watano (5) wamehamishwa Hospitali ya Maweni kwaajili ya matibabu. Treni iliendelea na safari kuelekea mikoa ya Tabora, Dodoma, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.
Shirika linawapa pole majeruhi na linaendelea na jitihada za kuwahudumia. Hakuna taarifa ya vifo vilivyotokana na ajali, taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.