Rapa kutoka nchini Marekani, Fatman Scoop amefariki dunia baada ya kudondoka jukwaani akiwa anapafomu, tukio lililotokea Connecticut, Marekani Ijumaa usiku.
Fatman alikuwa akipafomu kwenye tamasha la bure la Green & Gold Party lililofanyika Hamden, Connecticut ambapo dakika za mwisho alionekana akiwachangamsha mashabiki jukwaani kwa kuwaambia wapige kelele ambapo ghafla alidondoka nyuma ya meza ya DJ ambapo baadaye alikimbizwa hospitali lakini alipofikishwa, madaktari walieleza kwamba tayari amefariki dunia.
Fatman aliyefariki akiwa na umri wa miaka 53, alipata umaarufu baada ya kufanya kolabo na wasanii Missy Elliott na Ciara mwaka 2005 kwenye ngoma ya Lose Control na baadaye kufana kolabo na Mariah Carey kwenye ngoma ya It’s Like That.
“Sauti na energy ya Fatman Scoop imechangia kuzifanya nyimbo nyingi kuhit na kuwafurahisha mashabiki kwa zaidi ya miongo miwili, mchango wako ni mkubwa na kamwe hautasahaulika,” aliandika Missy Elliot kwenye akaunti yake ya mtandao wa X (Twitter).