Katika kuhakikisha askari wa Kike wanakuwa imara na mahiri katika kila nyanja wanazohudumu Suala la kujengewa umahiri katika ulengaji wa Shaba kwa askari hao likatolewa na wabobezi wa shabaha (Sniper) kutoka Jeshi la Polisi Nchini Marekani.
Miongoni mwa askari wa kike waliopata mafunzo ya ukupigaji shabaha nchini humo ni Koplo wa Jeshi la Polisi Kutoka Nchini Tanzania CPL Salome Masanyiwa ambaye amepata fursa hiyo amebainisha kuwa mafunzo hayo yamemjenga na kumuongezea umahiri katika upigaji wa shabaha tofauti na kipindi cha Nyuma.
Aidha CPL Salome amesisitiza kuwa mafunzo hayo yamemuongezea utaalam katika matumizi ya silaha na ulengaji wa shabaha huku akiweka wazi kuwa anakwenda kupeleka ujuzi huo alioupata kwa askari wengine kutoka nchini Tanzania ambao hawakupata fursa ya mafunzo hayo.