Mamlaka ya China inachunguza kisa cha mzee aliyefariki siku 13 baada ya kung’olewa meno 23 na kuwekewa vipandikizi 12 siku hiyo hiyo katika kliniki ya meno.
Bi. Shu, mkazi wa Jiji la Yongkang, katika Mkoa wa Zhejiang nchini China, hivi majuzi aliwasilisha malalamiko kwenye Ofisi ya Afya ya Manispaa dhidi ya kliniki ya meno ya eneo hilo baada ya kifo cha baba yake.
Mwanamke huyo aliwasilisha ushahidi kwamba mzazi wake aling’olewa meno 23 na kupandikizwa meno mapya 12 katika kipindi kimoja, jambo ambalo anadai lilisababisha kifo chake kisichotarajiwa siku 13 baadaye.
Bi Shu aliambia mamlaka kwamba babake alipata maumivu makali katika siku 13 zilizopita za maisha yake, kabla ya kupata mshtuko mbaya wa moyo mnamo Agosti 28.
Sasa mwanamke huyo anataka waliohusika wafikishwe mahakamani.