Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Maafisa waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na viongozi wa vyombo vya usalama wa Wizara hiyo kutekeleza kwa vitendo na kuiishi falsafa ya R nne (4R) ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Amesema kuwa ni muhimu kuifahamu vyema falsafa hiyo ya Rais Dkt. Samia na kuitekeleza kwa vitendo. “Nina imani kubwa kwamba uongozi wa juu wa Wizara umeielewa vizuri falsafa hiyo, na semina hii elekezi ni ushahidi tosha wa kuitekeleza kwa vitendo”
Amesema hayo leo (Ijumaa, Septemba 06, 2024) wakati alipofungua Semina elekezi kwa viongozi waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Weruweru River Lodge, mkoani Kilimanjaro.