Klabu ya Azam inayoshiriki ligi kuu ya NBC imeendelea kuonyesha ukubwa wake kwa mafanikio ya kiuwekezaji yanayoendelea kufanyika klabuni hapo. Klabu hiyo yenye makao makuu Chamazi jijini Dar es salaam inamiliki uwanja wenye hadhi ya kimataifa ukivizidi viwanja vingi vya Africa Mashariki.
Uwanja wa Azam Complex ulifanyiwa maboresho kwa kuwekewa majukwaa yenye viti na kubeba watazamaji 10,000 ukiwa na Mabango ya kisasa ya kutangaza biashara pamoja na nyasi bandia kwenye eneo la kuchezea. Ubora wa uwanja huo umepelekea Uwanja huo kujumuishwa kwenye orodha ya viwanja viwili bora vya Tanzania vinavyofaa kutumika kwenye michuano ya CAF inayoendelea msimu.
Klabu ya Yanga inautumia uwanja wa Azam Complex kwa mechi za nyumbani na inalazimika kulipa kiasi cha shilingi milioni 5.9 kwa kila mechi sawa na shilingi milioni 88.5 kwa mechi 15 za ligi ya NBC
Timu Za Ndani(Tanzaniaย )
Mazoezi (Mchana):600,000
Mazoezi (Usiku):1,500,000
Mechi (Mchana au Usiku):5,900,000.
Timu za nje ya Tanzania.
Mazoezi (mchana au Usiku):$ 1,000 sawa na 2,357,000.
Mechi (Mchana au Usiku):$ 5,000 sawa na 11,785,000.