Wagombea wawili wa uchaguzi wa rais nchini Algeria ambao walishindwa na rais aliye madarakani Abdelmadjid Tebboune waliwasilisha rufaa kwenye Mahakama ya Katiba Jumanne, kupinga matokeo ya muda ya uchaguzi huo.
Abdelaali Hassani, kiongozi wa chama cha Kiislamu chenye msimamo wa wastani, the Movement of Society for Peace, alikuwa wa kwanza kuwasilisha rufaa yake.
Alisema siku moja kabla “alishindwa mpambano lakini sio vita” na ametupilia mbali matokeo akisema ni “ulaghai”.
Youcef Aouchiche, kiongozi wa chama cha kisosialisti cha mrengo wa wastani wa kushoto (FFS), baadaye aliwasilisha rufaa, akiishtumu mamlaka ya uchaguzi ANIE kwa “kughushi” matokeo ya uchaguzi wa Septemba 7.
ANIE Jumapili ilimtangaza Tebboune kuwa mshindi kwa kupata asilimia 94.5 ya kura, huku Hassani akipata asilimia 3.17 na Aouchiche asilimia 2.16.