Kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi wa Kenya, Gilbert Masengeli amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela, kwa kosa la kudharau Mahakama.
Uamuzi huo umetolewa hii leo Septemba 13, 2024 na Mahakama ya juu ya Kenya kupitia Jaji Lawrence Mugambi baada ya Kaimu IGP huyo kutoheshimu wito wa Mahakama kwa mara saba mfululizo.