Usikilizwaji wa muziki wa Msanii wa Marekani, Sean Diddy Combs umeongezeka katika mitandao ya kusikilizia na kupakua muziki duniani tangu kutangazwa kukamatwa kwake Jijini New York September 16 2024 kwa mashtaka matatu ya jinai yanayohusu biashara ya ngono na ulaghai.
Mitandao ya Marekani imeripoti kuwa idadi ya Watu wanaofuatilia na ku-stream kazi za Msanii huyo imeongezeka kwa wastani wa asilimia 18.3% katika kipindi cha Septemba 13 hadi 19 mwaka tofauti na wiki za awali kabla hajakamatwa, takwimu hizi ni kwa mujibu wa Kampuni ya Data na uchanganuzi ya Luminate ya Los Angeles, California.
Ikumbukwe kuwa mauzo ya Mwimbaji R-Kelly yalipanda kwa asilimia mia tano kumi na saba (517%) mwaka 2021 baada ya kutolewa makala maalum ya Lifetime Documentary iliyokua inazungumzia matendo yake mabaya dhidi ya Wanawake na Wasichana wadogo.
Hadi sasa Diddy ambaye November 2024 atatimiza umri wa miaka 55, anashikiliwa katika Gereza lililopo New York Marekani.
Chanzo MillarAyo