TAJIRI wa India Ratan Tata amefariki dunia Oktoba 9, 2024 Mumbai, Maharashtra, India akiwa na umri wa miaka 86, imesema Tata Group, muungano wa makampuni alioongoza kwa zaidi ya miaka 20.
Tata alikuwa mmoja wa viongozi wa biashara wanaotambulika kimataifa nchini India.
Kundi la Tata ni mojawapo ya makampuni makubwa zaidi ya India, yenye mapato ya kila mwaka ya zaidi ya $100bn (£76.5bn).
Katika taarifa ya kutangaza kifo cha Tata, mwenyekiti wa sasa, Natarajan Chandrasekaran alimtaja kama kiongozi wa kipekee.
Natarajan Chandrasekaran aliongeza kwa niaba ya familia ya Tata, ninatuma salamu zetu za rambirambi kwa wapendwa wake.
Waziri wa Biashara wa Uingereza Jonathan Reynolds alisema kwa heshima kwamba Tata alikuwa nguzo muhimu katika ulimwengu wa biashara.
Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi amesema Tata alikuwa kiongozi mwenye maono na binadamu mwenye huruma.
Alisema kwenye X: “Alitoa uongozi thabiti kwa moja ya nyumba kongwe na za kifahari zaidi za biashara nchini India.