Msemaji mkuu wa jeshi la Nigeria Edward Buba amesema kwamba jeshi la Nigeria limefanya operesheni tofauti za kijeshi nchini kote, ambapo limeua watu wanaoshukiwa kuwa na silaha zaidi ya 165 na kuwakamata wengine 238 katika wiki iliyopita.
Akiongea na wanahabari mjini Abuja, Bw. Buba amesema wanajeshi hao walipata maficho ya vikundi vya wahalifu, wakaharibu kambi zao za vifaa, na kufanya operesheni zilizofaulu katika maeneo mengi ya nchi hiyo.
Amesema kuwa katika kipindi hicho, raia 188 waliotekwa na magenge ya wahalifu waliokolewa na wanajeshi, na kwamba silaha 153 na risasi zaidi ya elfu mbili za aina mbalimbali pia zilipatikana. Amesema wanajeshi wa Nigeria wanaifanyia kazi mikakati mipya ya kulinda vizuri taifa na raia.
Chanzo – MillardAyo