Papa Francis Ijumaa Oktoba 11, 2024 amekutana na kuzungumza na Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine ambaye baadaye amepata nafasi ya kukutana na kuzungumza pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano na Mashirika ya Kimataifa.
Mazungumzo kati ya Papa Francis na mgeni wake, yamejikita hasa kuhusiana na vita inayoendelea kati ya Ukraine na Urusi
Papa amesema siasa inayohitajika katika kujenga udugu wa kibinadamu na urafiki wa kijamii, inapania pamoja na mambo mengine kukuza na kudumisha amani.
Hii ni mara ya tatu kwa Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine kukutana na kuzungumza na Papa Francis, kwani mara ya kwanza ilikuwa ni Februari 8, 2020, mazungumzo yaliyodumu dakika arobaini na tano.
Mara ya pili ilikuwa ni mjini Puglia, Kusini mwa Italia wakati wa mkutano wa Viongozi Wakuu wa Kundi la Nchi Saba zilizoendelea zaidi kiviwanda duniani, G7.
Chanzo – Global Publishers