Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 14, 2024 ameshiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya Hayati Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa la Mt. Francis Xavier Nyakahoja Jijini Mwanza.
Katika Ibada hiyo Viongozi mbalimbali wa Kitaifa wamehudhuria akiwemo Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi, Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko.