Umoja wa wananfunzi wa vyuo vya Kati na vyuo vikuu seneti ya Dar wa salaam wamezindua kampeni ya “Samia for us” yenye lengo la kutangaza kazi za maendeleo zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya rais dkt.Samia Suluhu na wasaidizi wake .
Akizungumzia uzinduzi wa kampeni hiyo mwenyekiti wa taasisi hiyo ya “Samia for us”ndugu Geofrey kiliba amesema wao kama vijana wasomi ambao wamekuwa wanufaikaji wakubwa na kazi ya Rais Samia wameona ipo haja yakupaza sauti zao na kuiambia jamii mema yanayofanywa na Dkt.Samia.
Ameyasema hayo Leo tarehe 13 mwezi wa kumi katika ukumbi wa anatoglou jijini Dar es salaam ambapo wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali walipata fursa ya kuhudhuria tukio hilo.
“Kampeni hii imelenga hasa kumuunga mkono rais samia kwa mambo makubwa na mazuri anayofanya katika taifa letu , sisi kama vijana wasomi tunataka kutumia maarifa yetu kuiambia jamii mambo ya kweli yanayofanywa na serikali yetu na tupo tayari kupaza sauti zetu katika mazingira yeyote”
Kwa upande wake Katibu mkuu msaidizi wa taasisi hiyo Bibi Prisca Noel amesema sauti za Vijana bado hazitoshi kwenye kusema mazuri ya Rais samia hivyo taasisi ya samia for us wameamua kulibeba jukumu hilo ili wananchi wajue serikali Yao ipo kazini.
Chanzo – MillardAyo