Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (Mb.) Kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) ameshiriki kwenye maadhimisho ya miaka 10 ya Jumuiya ya Ushirikiano kati ya Tanzania na China yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tarehe 30 Novemba, 2024 ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
Viongozi wengine walioshiriki Maadhimisho hayo ni Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Kayanza Peter Pinda na Balozi wa China hapa nchini, Mhe
Chen Mingjian.
Mhe. Waziri Mkuu amesema Tanzania inathamini ushirikiano wake na China katika kukuza maendeleo na kwamba ukuaji wa ushirikiano huo umechangia kukua kwa maendeleo ya viwanda nchini, kutengeneza ajira, ujenzi wa miundombinu na kuleta ustawi wa watanzania kwa ujumla.