Mchezo namba 184 (YANGA SC V s SIMBA SC) ulioghairishwa kuchezwa tarehe 8 Machi, 2025 sasa utachezwa tarehe Juni 15, 2025 siku ya Jumapili saa 11:00 jioni kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa.
YANGA SC wamebainisha kuwa msimamo wao kuhusu mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba SC uliotarajiwa kuchezwa Machi 8 2025 upo palepale.
Yanga imebainisha kuwa msimamo wao upo palepale kuhusu mchezo huo licha ya CAS kutoa majibu ya kesi yao kuhusu kesi ya mchezo huo.
Taarifa iliyotolewa na Yanga SC Mei 5 2025 imeeleza namna hii: “Uongozi wa Yanga unapenda kuutarifu umma kuwa umepokea majibu kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo, (CAS) kuhusu kesi namba CAS 2025/A/11298.
“CAS imeilekeza Yanga SC kurudi kwanza kwenye Kamati za ndani za soka ili kushughulikia kesi hiyo kabla ya kurudi kwao kwa ajili yah atua za rufaa.