Watu watatu wa familia moja wamefariki dunia katika hali ya kutatanisha wakati wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaaya Mkoa wa Manyara huku sababu ya vifo vyao ikiwa bado haijajukukana.
Kaimu Mratibu wa Matibabu Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara, Mathias Kimaro amesema Watu hao ni mama pamoja na watoto wake wawili ambao walifikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara kwa nyakati tofauti mwanzoni mwa wiki la Juni 2025.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, Ahmed Makarani ametoa angalizo kwa Wananchi kutoa taarifa juu ya matukio ya vifo vyenye utata mkoani humo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kKijiji cha Nakwa kilichopo Wilayani Babati amesema tukio hilo ni kubwa kuwahi kutokea na limegusa mioyo ya watu.