Taarifa hizo ni kwa mujibu waĀ vyanzo vya kitabibu kwenye ardhi hiyo ya Wapalestina.
Kulingana taarifa kutoka eneo hilo, kwa jumla Wapalestina 69 wameuawa kutwa nzima jana kwenye maeneo tofauti ya Ukanda wa Gaza.
Wale waliouawa wakitafuta mahitaji muhimu walikuwa kwenye kituo cha kusambaza misaada kinachoendeshwa na wakfu wenye utata unaoungwa mkono na Israel na Marekani kwa utoaji misaada ndani ya Gaza.
Wakfu huo umekanusha taarifa za vifo au majeruhi karibu na vituo vyake vya kutoa misaada. Hata hivyo mikanda ya video imeonesha maafisa wa jeshi wakiwalenga Wapalestina kwa risasi na baadhi ya miili ya watu ikiwa chini.
Umoja wa Mataifa umeukosoa mfumo huo wa sasa wa usambazaji misaada kupitia wafku wa GHF ukisema haufanyi kazi.