
STAA wa mitandao na mrembo maarufu, Ester Simba maarufu kama Caren Simba amevunja ukimya na kufafanua kuhusu madai ya kuhusishwa kimapenzi na mchezaji wa Klabu ya Yanga, Pacome Zouzoua.
Akizungumza kwa uwazi, Caren amesema amedai hana uhusiano wowote wa kimapenzi na nyota huyo wa Yanga, bali wao ni marafiki wa kawaida waliokutana kupitia kazi na mashabiki wa kazi za kila mmoja.
“Skendo ambayo naichukia ni hii ya kuambiwa nimewahi kutoka kimapenzi na Pacome. Jamani mimi ni shabiki yake, yeye ni shabiki yangu kwenye kazi za sanaa.

Hivyo nakuwa naye karibu sababu ya kuzoeana na siyo kimapenzi,” amesema Caren.
Ameongeza kuwa licha ya kuwa na ukaribu, mara kadhaa Pacome amekuwa akimwalika sehemu za burudani kama vile disco au mikusanyiko ya starehe, jambo ambalo watu wamekuwa wakilitafsiri vibaya. ,” alisisitiza.
