
Ripoti ya shirika lisilo la kiserikali la “DESC”, mwezi Aprili mwaka jana, ilidai kwamba rasilimali za madini ya mkoa wa zamani wa Katanga inachimbwa kwa njia ya fujo na kuporwa kimfumo, ikishutumu familia ya rais Félix Tshisekedi kwa uporaji wa madini hayo.
Ripoti hiyo inataja shughuli za uchimbaji madini mikononi mwa takriban watu kumi wa familia ya rais, akiwemo kaka yake, mama yake na mkewe. Tisa kati yao wana uraia wa Ubelgiji. Matukio ya hivi punde katika kesi hii ni malalamiko rasmi yaliyowasilishwa kwa mahakama ya Ubelgiji siku ya Jumanne, Julai 8.
Mwezi Aprili mwaka huu, shirika lisilo la kiserikali la DESC, jukwaa la mashirika ya kiraia kwa ajili ya kukuza na kutetea Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, lilitoa ripoti yenye kichwa “Maono ya Mkuu wa Nchi katika migodi; Kuna hatua moja tu kati ya uvamizi wa maeneo ya uchimbaji madini ya makampuni binafsi na kuhalalisha uchimbaji madini haramu.”
Kufuatia ufichuzi uliomo kwenye faili hiyo, malalamiko ya kurasa 80 yaliwasilishwa kwa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Shirikisho huko Brussels siku ya Jumanne, Julai 8. Hati hii inaitwa “kulaani vitendo,” vinavyofanywa na watu tisa kutoka familia ya rais Félix Tshisekedi wanatuhumiwa kupora rasilimali za madini za Katanga kwa manufaa yao binafsi.
Ufisadi, Utakatishaji wa Pesa, Ubadhirifu, na Makosa ya Jinai ya Kifedha
Kwa mujibu wa mwanaharakati Jean-Pierre Muteba, msemaji wa mashirika yanayopambana na ufisadi, uchimbaji madini haramu, ufujaji na utakatishaji fedha, ripoti nyingi nchini Kongo hazijapata majibu maridawa, hivyo basi malalamiko haya ya kisheria dhidi ya watu hawa tisa, ambao wote ni raia wa Ubelgiji. Ufisadi, utakatishaji fedha, ufujaji na makosa ya jinai ya kifedha yote yanadaiwa katika malalamiko yaliyowasilishwa Ubelgiji kwa niaba ya kundi la mawakili wa kutoka Katanga na Bernard Maingain.
Wamekataa kutaja majina ya watu tisa wa familia ya rais wa Kongo ambao wanalengwa, kwa vile wanataka kuruhusu sheria ifuate mkondo wake kwa matumaini kwamba hati za kukamatwa zinaweza kutolewa.
