
Mvutano mkubwa umeibuka kati ya Shirikisho la Soka la Hispania (RFEF) na klabu ya Barcelona baada ya shirikisho hilo kulalamika kuwa halikujulishwa mapema kuhusu hali ya kiafya ya nyota chipukizi Lamine Yamal.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya RFEF, Yamal alifanyiwa matibabu ya radiofrequency kutokana na maumivu ya nyonga siku hiyo hiyo ambayo kambi ya timu ya taifa ya Hispania ilianza bila taarifa yoyote kutolewa kwa madaktari wa timu ya taifa.
Shirikisho hilo limesema lilipokea ripoti ya kitabibu usiku huo huo, ikipendekeza mapumziko ya siku 7 hadi 10, jambo lililowalazimu kumruhusu Yamal arudi nyumbani kwa ajili ya afya yake.
“Nimeshtushwa,” alisema kocha wa Hispania Luis de la Fuente, akielezea kutoridhishwa na hatua ya Barcelona kutowapa taarifa mapema.
Kwa sasa, Lamine Yamal hatacheza mechi yoyote na Hispania, na amerudi Barcelona kwa ajili ya mapumziko ya wiki mbili ili kuimarisha hali yake kabla ya kurejea uwanjani.
