
Na Nyamiti A, Nyamiti
Maafisa Mipango wa Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga wameendelea na mafunzo ya uibuaji wa Miradi ya Maendeleo kwa wataalam wa ngazi za Kata kupitia Mfumo wa O&OD Ulioboreshwa, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2027/2028.

Kufuatia mafunzo hayo kuzinduliwa rasmi Novemba 18, 2026 katika Kata ya Malunga, leo Novemba 19, kata zilizopatiwa mafunzo hayo ni Nyandekwa, Iyenze, Isagehe, Mondo, Zongomela, Kagongwa, Mhungula, Kilago na Nyihogo.
Zoezi hilo linatarajiwa kuendelea katika kata zingine ambazo hazijafikiwa, ambazo ni Mhongolo, Busoka, Majengo, Nyahanga, Kinaga, Mwendakulima, Ngogwa, Wendele na Kahama Mjini.

Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuimarisha ushiriki wa wananchi katika mchakato wa maendeleo ili kuhakikisha miradi inayopangwa inatokana na mahitaji na vipaumbele halisi vya jamii.


