
Na Nyamiti A, Nyamiti
Tukio la kusikitisha limetokea Mtaa wa Chapulwa, Kata ya Mwendakulima, Manispaa ya Kahama, baada ya mwili wa kichanga kinachokadiliwa kuwa na umri wa siku tatu kukutwa ndani ya kisima kilichopo kwenye familia ya Mzee Masele Nzengula Shija.
Taarifa za tukio hilo zimetolewa na mmoja wa wanafamilia hiyo, Paschal Masele, baada ya kubaini uwepo wa kichanga hicho ndani ya kisima asubuhi ya leo Novemba 22, 2026.
Paschal alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Chapulwa, Bahati Kitinde, ambaye naye alitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi Kahama.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Mtaa huo Amethibitisha Uwepo wa tukio hilo na kuongeza kuwa wanaendelea na juhudi za kumsaka Mtuhumiwa wakishirikiana na Jeshi la polisi.
Jeshi la Polisi limefika eneo la tukio na kuutoa mwili huo wa kichanga ambacho tayari kilikuwa kimefariki, na kuondoka nao kwa ajili ya taratibu zaidi za kisheria.
Hadi sasa haijafahamika ni nani aliyehusika na tukio hilo, huku uchunguzi wa Polisi ukiendelea kubaini chanzo na wahusika.
