Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Farida Mgomi amekabidhi Mashine ya Photocopy katika Shule ya Sekondari Shinji ambayo imetolewa na Kampuni ya kusambaza umeme DERM ELECTRICS LTD ambayo ilikuwa kero shuleni hapo tangu kuanzishwa Januari ,2023.
DC Mgomi amekabidhi Mashine hiyo Oktoba 9,2023 shuleni hapo ikiwa ni shughuli ambayo imefanyika wakati wa ziara ya kusikiliza kero za wananchi kwenye mikutano ya hadhara.
Mgomi amesema alipokea ombi kutoka Kwa viongozi wa shule hiyo ambapo alizungumza na kampuni hiyo ambayo imefanikiwa kutoa mashine photocopy yenye uwezo wa kuscan na kuprint Kwa wakati mmoja.
Hakikisheni mnaitunza mashine hii ili iweze kufanya kazi kwa mda mrefu na kutimiza ndoto kwa kufanya maandalizi ya mitihani ya mara Kwa mara shuleni hapo na nyaraka mbalimbali za shule”, amesema Mgomi.
Mgomi amewataka wakandarasi wanaofanya kazi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo wilaya ya Ileje kutoa msaada kwenye idara mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kurejesha fadhila Kwa wananchi wa Ileje.
“Tumefanikiwa kupata vifaa hivi, tuhakikishe tunavitumia Kwa kuleta mabadiliko na kuvitunza na kuleta mabadiliko chanya Kwa kufanya vizuri kwenye taalumua ngazi ya wilaya na taifa”, amesema Mgomi
Akimkabidhi mashine hiyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ileje mwakilishi wa Kampuni ya kusambaza umeme DERM ELECTRICS LTD Ally Mnyanga amesema kutoa msaada kumetokana na ombi alilolipokea li kutatua changamoto ya kuandaa shughuli za shule ikiwepo kuandalia mitihani na nyaraka za shule Hali ambayo itapunguza gharama.
Mkuu wa Shule hiyo Novatus Nicholaus amesema kupatikana kwa Mashine wanahaikisha wataendelea kumsaidia Mkuu wa Wiaya kuhakikisha Wilaya ya Ileje inakuwa kwenye Sekta ya Elimu ,Mazingira na sekta nyingine
Ikumbukwe Shule hiyo ni Shule mpya ya Sekondari ambayo imejengwa na Serikali kwa lengo la kuwarahisishia wanafunzi wa Kijiji cha Shinji kutembea umbali mrefu kupata huduma ya masomo Shule ya Sekondari Mbebe.