
Karim Boimanda, Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB) amebainisha kuwa sherehe za kukabidhi taji ya ligi kuu zitafanyika Juni 25 baada ya mchezo wa Yanga dhidi ya Simba utakaochezwa Uwanja wa Benjamini Mkapa.
Yanga ni mabingwa watetezi wakiwa wamejenga ufalme wao kwa misimu mitatu huku Simba ikipambana kuvunja rekodi hiyo.Kwenye msimamo Yanga nafasi ya kwanza na pointi 79 inafuatiwa na Simba nafasi ya pili na pointi 78.
Yanga ili atawe ubingwa ana hitaji sare ama ushindi ni faida kwake na Simba chaguo lake ni moja ili atwae ubingwa ni kuvuna pointi tatu mazima.
Historia inaonesha kuwa hii ni kwa mara ya pili kwa miamba hiyo kukutana katika mchezo wa maamuzi ya ubingwa wa ligi baada ya ule wa mwaka 1985.
