Papa na Askofu Mkuu wa Canterbury wamefanya ziara ya kigeni pamoja kwa mara ya kwanza katika historia, akijumuika na kiongozi mkuu katika Kanisa la Scotland.
“Hii itakuwa ni ziara ya kihistoria baada ya karne nyingi za migawanyiko, viongozi wa sehemu tatu tofauti za Kanisa wanakutana kwa namna isiyo na kifani,” anasema Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby.
Dhamira yao ni kuleta matumaini na kuhimiza viongozi kutafuta amani ya kudumu nchini Sudan Kusini.
“Tunaomba kwamba ziara hii iwe chachu kwa viongozi wa Sudan Kusini kuzingatia kile kinachowaunganisha na sio kinachowatenganisha kwa kuwa wote wanapendwa kwa usawa machoni pa Bwana,” anasema Mchungaji Iain Greenshields, Msimamizi wa Jenerali. Mkutano wa Kanisa la Scotland.
Taifa hilo changa zaidi duniani limekumbwa na vita vya umwagaji damu vya wenyewe kwa wenyewe tangu viongozi wake walipotofautiana kuhusu udhibiti wa nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta mwaka 2013, miaka miwili tu baada ya uhuru wake kutoka kwa Sudan.
Zaidi ya asilimia 60% ya wakazi wa Sudan wanakadiriwa kuwa Wakristo, hasa wa madhehebu ya Kikatoliki, Anglikana na Presbyterian, ingawa vita hivyo vimepiganwa kwa misingi ya kikabila na si ya kidini.