Uamuzi huo umefikiwa na Mawaziri wa Nchi za Afrika, baada ya Mkutano wa pili uliofanyika jijini Nairobi ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA)
Katibu Mkuu wa AfCFTA, Wamkele Mene, amesema uamuzi wa kuzuia biashara ya mitumba ni hatua muhimu ya kuhimiza Uongezaji Thamani na Kulinda Maendeleo ya Viwanda pamoja na kuhakikisha Afrika haiwi jalala la nguo za Mtumba kutoka nje
Hii ni mara ya pili kufanyika makubaliano haya, mwaka 2015 Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) walizuia biashara hiyo lakini utekelezaji wake haukufanyika. Nchi ya Rwanda pekee imefanikiwa kuzuia biashara hiyo