Na Evelyne Ernest
Hamidu Musa, Mwanafunzi wa Kidato cha Pili Katika Shule ya Sekondari Rutunga iliyopo Kata ya Kahororo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, amepoteza maisha wakati akiogelea ndani ya Ziwa Victoria jioni ya Juni 11 Mwaka huu.
Kaimu Kamanda wa Mkoa huo, Maketh Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo wakati akizungumza na Divine Fm, amesema Hamidu amekutwa na mauti hayo Jioni ya Saa Kumi na Mbili katika fukwe zilizopo eneo la Nyamkazi iliyopo Kata ya Miembeni, Manispaa hiyo.
Kaimu Kamanda Msangi ametumia nafasi hiyo kuwataka wazazi na walezi kuwa waangalifu kwa watoto pindi wanapoenda ziwani kuongelea kwa kuwapa elimu juu ya tadhari za maji.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Erasto Siima amesema kwa sasa wanafunzi wapo majumbani katika kipindi cha likizo ndefu, na Tangu Januari hadi Mei walikuwa mikononi mwa walimu hivyo ni vyema kila mzazi au mlezi kutimiza majukumu yao kwa kuwalea watoto wao vizuri na kuwafundisha maadili mema.