Na Lucia Nyamasheki
Akinababa wametakiwa kusimamia na kutunza familia zao kikamilifu bila kuwategemea wake zao kwani wao ni vichwa vya familia.
Hayo yameelezwa leo 12 Juni, 2023 na Askofu Mkuu wa Kanisa la Christian Gospel Rivival Assembly (CGRA), Jovin Mwemezi, lililopo Shunu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga alipokuwa akifundisha katika kipindi cha Pata Ufahamu kuwa akinababa wengi hawahudumii familia zao kikamilifu kwa kuangalia kipato cha wake zao jambo ambalo si sahihi kwani wanawake ni wasaidizi na si watunzaji wala waongoza familia.
Pia Askofu Mwemezi amewataka wajue kutafuta na kutumia pesa huku wakizingatia kula vyakula vya kuwapa afya na nguvu kitu ambacho wanaume wengi hawazingatii bali wanawekeza sehemu mbalimbali huku wakidhoofika kiafya.
Mbali na hayo Askofu Mwemezi amewashauri watu wamwamini na kumkiri Yesu Kristo ili wawe wenye haki na watende haki kwani hatua na mafanikio ya mtu huimarishwa na Bwana.