Na Nyamiti Alphonce – Kahama, Shinyanga
Akifungua mafunzo hayo msaidizi wa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali ( AAG) Bi. Anna Massanja Amesema mafunzo hayo yatawajengea uwezo Waandishi katika kuripoti kazi za ukaguzi wa Mali za Umma.
Hata hivyo Bi. Massanja ameongeza kusema kuwa jamii ina haki ya kutambua majukumu ya Ofisi ya CAG na namna inavyotekeleza majukumu yake.
Baadhi ya waandishi walioshiriki mafunzo hayo Shaban Njia na Kareny Masasi wamesema kutokana na mafunzo hayo yamewajengea uwezo katika kutekeleza majukumu yao na uwezo wa kuielimisha jamii kuhusiana na masuala ya ukaguzi.